

11 June 2025, 11:27 am
Kiasi cha shilingi bilion 5.71 kimetolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kata ya Bunda stoo katika kipindi cha miaka mitano yaani 2021 na 2025.
Na Adelinus Banenwa
Kiasi cha shilingi bilion tano milioni miasaba na kumi lakisaba na hasini na nane miatatu arobaini na moja (5,710,758,341) kimetolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwa kata ya Bunda stoo katika kipindi cha miaka mitano yaani 2021 na 2025.
Hayo yamebainishwa Jumanne june 10 , 2025 kupitia taarifa ya diwani wa kata ya Bunda stoo Mhe Flavian Chacha Nyamageko mbele ya wajumbe wa baraza la maendeleo la kata ya Bunda stoo lililoketi ambapo pamoja na mambo mengine baraza hilo lilikuwa na kazi ya kumuaga diwani huyo baada ya kufanya naye kazi katika kipindi ambacho yeye alikuwa diwani na mwenyekiti wa baraza.
Akisoma taarifa mbele ya wajumbe wa baraza la maendeleo la kata kwa niaba ya diwani, mwenyekiti wa mtaa wa Butakare Sebastian Chacha Masugo amesema fedha hizo zimefanikisha kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya Afya , Maji, Elimu, Barabara, Umeme miongoni mwa miradi mingine.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Mhe Flavian Chacha amelishukuru baraza hilo kwa moyo wa upendo waliouonesha kwake katika kipindi chote ambacho amefanya nao kazi, huku akitambua mchango wao kama wajumbe kwa juhudi walizofanya kuwezesha fedha zilizoletwa na serikali zinatekeleza miradi husika kwa maslahi ya wananchi.
Baraza hilo kwa kutambua mchango wa diwani huyo pia walitoa zawadi mbalimbali kwa mwenyekiti wao huku Mhe Nyamigeko akitamka wazi kuwa baada ya baraza la madiwani kuvunjwa atakwenda kuchukua fomu kutetea nafasi yake,