Mazingira FM

Getere ampongeza mwenyekiti wa kijiji kusimamia upatikanaji wa sekondari

8 January 2024, 7:58 am

Mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniphas Mwita Getere

Mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniphas Mwita Getere amempongeza mwenyekiti wa kijiji cha Nyaburundu Hamisi Said Madoro kwa kusimama kidete ili kupata shule ya sekondari Nyaburundu.

Na Adelinus Banenwa

Mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniphas Mwita Getere amempongeza mwenyekiti wa kijiji cha Nyaburundu Hamisi Said Madoro kwa kusimama kidete ili kupata shule ya sekondari Nyaburundu.

Mhe Getere ameyasema hayo katika kikao na wananchi wa kijiji cha Nyaburundu alipofika leo kuzungumza nao na kusikiliza kero zao.

Aidha Mhe Getere amesema kwa sasa shule nyingi za msingi katika jimbo la Bunda zina hali mbaya hivyo amewataka wakazi wa Nyaburundu kupongeza jitihada za serikali kwa kuwaletea madarasa mengi ya shule ya msingi ambayo yanajengwa katika shule yao ya Nyaburundu.