Mazingira FM

Mbunge Bulaya afadhili vifaa vya michezo Bitaraguru FC

17 June 2026, 7:08 pm

Katibu wa mbunge Musa Hussen akikabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa Bitaraguru FC

Wakati mwingine wachezaji hao walikuwa wakicheza vifua wazi kutokana ana uhaba wa jezi hivyo msaada huo wa jezi utasaidia kwa kiasi kikubwa vijana hao kuongeza morali.

Na Adelinus Banenwa

Katika kuunga mkono maendeleo ya michezo kwa vijana, Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya, amekabidhi seti ya jezi pamoja na mpira kwa timu ya vijana ya Bitaraguru iliyopo Kata ya Kabasa. Hatua hiyo inalenga kuimarisha mazingira ya vijana kushiriki katika shughuli za michezo, kuibua vipaji vyao na kuwajengea ari ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

Katibu wa mbunge Musa Hussen akikabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa Bitaraguru FC

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Katibu wa Mbunge huyo, kwa niaba yake, aliwataka vijana kuendelea kutumia michezo kama nyenzo muhimu ya kujenga afya bora, kukuza nidhamu na kutengeneza fursa mbalimbali za maendeleo. Amesisitiza kuwa michezo ina mchango mkubwa katika kuwawezesha vijana kufikia malengo yao na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii.

Kwa upande wao, vijana wa Bitaraguru kupitia kwa mwenyekiti wea vijana Alex Manyama amemshukuru Mhe. Bulaya kwa mchango huo, akieleza kuwa jezi na mpira waliopokea vitasaidia kuongeza morali, kuimarisha ushiriki wao katika mashindano mbalimbali na kuchochea maendeleo ya michezo ndani ya eneo lao. Wamesema msaada huo ni chachu ya kuendelea kujituma na kuonyesha vipaji vyao katika sekta ya michezo.

Sauti ya mwenyekiti wea vijana Alex Manyama

Naye mwenyekiti wa mtaa wa Bitaraguru Paulo Kasela amesema wakati mwingine wachezaji hao walikuwa wakicheza vifua wazi kutokana ana uhaba wa jezi hivyo msaada huo wa jezi utasaidia kwa kiasi kikubwa vijana hao kuongeza morali.

Aidha amemshukuru mhe mbunge kwa kuwapatia mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa sekondari ya bitaraguru ambapo ujenzi unaendelea

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Bitaraguru Paulo Kasela