Mazingira FM

Hatari ya kumwachia mtu ardhi kwa miaka 12 bila mkataba

15 August 2026, 7:41 pm

Wakili Aloyce Kajitanus wakati akitoa elimu ya sheria kupitia kipindi cha Ufahamu wa Sheria

Wananchi wanaotaka kumwachia mtu kutumia eneo lao wanapaswa kuweka makubaliano ili kuepuka migogoro.

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa kumruhusu mtu kukaa au kutumia eneo lako bila makubaliano rasmi kwa muda mrefu kunaweza kusababisha changamoto za kisheria kuhusu umiliki wa eneo hilo.

Hayo yameelezwa leo na Wakili Aloyce Kajitanus wakati akitoa elimu ya sheria kupitia kipindi cha Ufahamu wa Sheria kinachorushwa na Radio Mazingira FM, akisema watu wengi wamekuwa wakikumbwa na migogoro ya ardhi kutokana na kutofahamu sheria.

Sauti ya Wakili Aloyce Kajitanus

Wakili Kajitanus amesema wananchi wanaotaka kumwachia mtu kutumia eneo lao wanapaswa kuweka makubaliano ili kuepuka migogoro, huku akisisitiza kuwa kwa maeneo ya vijijini ni muhimu kutumia hati ya kimila inayotambulisha umiliki wa eneo, hata kama kuna mtu ameachiwa kulitumia.