Mazingira FM
Mazingira FM
24 August 2026, 10:50 am

Kumekuwepo changamoto kwa wakulima kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi na mwongozo kuhusu mfumo wa ununuzi wa mbegu katika msimu huu.
Na Adelinus Banenwa
Wito umetolewa kwa Serikali kutoa ufafanuzi kuhusu utaratibu wa uuzaji wa mbegu katika msimu mpya wa kilimo wa mwaka 2026/2027, ili wakulima kufahamu kama mbegu hizo zitauzwa kwa mfumo wa ruzuku au utaratibu mwingine.
Wito huo umetolewa na Kiberiti Amon, Mkurugenzi wa Kibe Vert Center, akizungumza kupitia kipindi cha kilimo kinachorushwa na Radio Mazingira FM.
Kiberiti amesema kumekuwepo changamoto kwa wakulima kutokana na kukosekana kwa ufafanuzi na mwongozo kuhusu mfumo wa ununuzi wa mbegu katika msimu huu, hali inayowafanya wakulima kukosa taarifa sahihi za kuwawezesha kujiandaa mapema.
Aidha, amewataka wakulima kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na mamlaka husika ili waweze kupanga shughuli zao za kilimo na kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Wito huo umetolewa wakati wakulima wakiendelea kujiandaa kwa msimu mpya wa kilimo wa mwaka 2026/2027.