Mazingira FM
Mazingira FM
3 October 2026, 7:55 pm

Amesema viongozi wa chama hicho wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi.
Na Edward Lucas
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche, amewataka wananchi kuendelea kukiunga mkono chama hicho, akisema hatua hiyo itasaidia kuendeleza jitihada za kupigania na kutetea maslahi ya nchi.
Heche ameyasema hayo leo wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Viwanja vya Malori, Mtaa wa Saranga, Kata ya Kabalimu, Bunda Mjini.

Amesema viongozi wa chama hicho wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia na kutetea maslahi ya wananchi.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Tanzania Bara, Amani Golugwa, amesema Tanzania inahitaji kutengeneza Katiba mpya ili kujenga taifa ambalo wananchi na viongozi wake wanawajibika, huku rasilimali za nchi zikitumika kwa manufaa ya wananchi.