Mazingira FM

Nyumba 301 Bunda zaathirika na mvua ya upepo

25 October 2026, 1:29 pm

Baadhi ya nyumba zilizoathirika an mvua ya upepo kata ya Kabasa

Magembe amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na tathmini ya athari zilizosababishwa na mvua hizo.

Na Adelinus Banenwa

Jumla ya nyumba 301 zimeathirika, huku nyumba 31 zikiwa zimebomoka kabisa kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali katika Kata ya Kabasa, Halmashauri ya Mji wa Bunda, mkoani Mara.

Akizungumza na redio ya Mazingira FM kuhusu athari za mvua hizo katika kata yake, Diwani wa Kata ya Kabasa, Mhe. Daniel Yona Magembe, amesema mvua hiyo ilinyesha Oktoba 22 mwaka huu, majira ya saa kumi jioni.

Baadhi ya nyumba zilizoathirika an mvua ya upepo kata ya Kabasa

Magembe amewataka wananchi kuendelea kuwa watulivu wakati serikali ikiendelea na tathmini ya athari zilizosababishwa na mvua hizo.

Aidha, amewahimiza wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya mvua zinazoendelea kunyesha, ikiwemo wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni kuhama na kwenda maeneo salama, pamoja na kuimarisha makazi yao ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

Sauti ya Mhe. Daniel Yona Magembe,