Mazingira FM
Mazingira FM
13 November 2026, 11:59 pm

Amewaelekeza viongozi katika ngazi mbalimbali kusimamia kikamilifu ulinzi na usalama wa watoto wa kike dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, hususan ukeketaji.
Na Adelinus Banenwa
Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Edward Gowele, amewaelekeza viongozi katika ngazi mbalimbali kusimamia kikamilifu ulinzi na usalama wa watoto wa kike dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia, hususan ukeketaji.
Gowele ametoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na vitendo hivyo, akisisitiza kuwa yeyote atakayebainika kujihusisha na ukeketaji atachukuliwa hatua kali za kisheria bila kupewa nafasi ya msamaha.
Ametoa kauli hiyo wakati wa kuhitimisha ziara ya viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, waliofika mkoani Mara kwa lengo la kutoa elimu na kuhamasisha jamii kuachana na vitendo vya ukatili pamoja na mila potofu za ukeketaji.

Aidha, imeelezwa kuwa vitendo vya ukeketaji huongezeka katika vipindi maalumu vya mwaka, hali inayohitaji viongozi, wazazi na jamii kwa ujumla kuongeza uangalizi na kuchukua hatua za mapema kuhakikisha watoto wa kike wanalindwa dhidi ya mila hiyo yenye madhara.