Mazingira FM

Mtelela ataka Bunda kumpa ushirikiano DAS mpya

6 October 2026, 1:18 pm

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salumu Mtelela kushoto akikabidhi ofisi kwa Katibu Tawala mpya, Shabani Manyama

Mafanikio yaliyopatikana ni ya pamoja, huku mapungufu akiyachukua kuwa jukumu lake binafsi.

Na Adelinus Banenwa

Aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salumu Mtelela, amewaaga viongozi, watumishi na wananchi wa wilaya hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka sita.

Mtelela aliyasema hayo wakati akikabidhi ofisi kwa Katibu Tawala mpya wa Wilaya ya Bunda, Shabani Manyama.

Amesema anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumwezesha kuhudumu kwa miaka sita, pamoja na hayati Rais John Magufuli kwa kumteua katika nafasi hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini katika kipindi chake cha uongozi.

Mtelela amesema miaka hiyo ilikuwa na nyakati za furaha na changamoto, huku akieleza kuwa amejifunza mengi. Aidha, amewashukuru wote kwa ushirikiano waliompa na kusema mafanikio yaliyopatikana ni ya pamoja, huku mapungufu akiyachukua kuwa jukumu lake binafsi.

Pia amewaomba viongozi, watumishi na wananchi wa Bunda kumpa ushirikiano Katibu Tawala mpya, Shabani Manyama, katika utekelezaji wa majukumu yake.

Sauti wakati wa makabidhiano