Mazingira FM
Mazingira FM
30 September 2026, 8:08 pm

Masuala ya afya, ustawi wa kiuchumi, heshima na ulinzi wa haki za wazee yanaendelea kuwa sehemu muhimu ya kuhamasisha jamii kuwajali na kuthamini mchango wao.
Na Adelinus Banenwa
Wazee katika Halmashauri ya Mji wa Bunda wametakiwa kuwa makini katika maamuzi ya kuoa mabinti wenye umri mdogo, wakitahadharishwa kuwa mahusiano hayo yanaweza kuwaathiri kiafya, kiuchumi na kijamii, ikiwemo kuachwa baada ya kutumia fedha zao.
Tahadhari hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Waryoba Juma, kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, ambayo huadhimishwa Oktoba Mosi kila mwaka. Amesisitiza umuhimu wa wazee kufanya maamuzi yenye kuzingatia ustawi wao, afya na usalama wa maisha yao.
Katika maadhimisho hayo, masuala ya afya, ustawi wa kiuchumi, heshima na ulinzi wa haki za wazee yanaendelea kuwa sehemu muhimu ya kuhamasisha jamii kuwajali na kuthamini mchango wao.