Mazingira FM

Baraza la madiwani Bunda TC laipa kongole idara ya elimu

26 September 2026, 7:46 pm

Baadhi ya Madiwani Halmashauri ya Mji wa Bunda

Katika mtihani huo, watahiniwa 2,845 walifanya mtihani, ambapo watahiniwa 2,399 sawa na asilimia 82 walifaulu kwa daraja la kwanza hadi la nne.

Na Juma Hangi

Idara ya Elimu Halmashauri ya Mji wa Bunda imepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa upimaji wa Kidato cha Nne wa Kanda ya Ziwa, ambapo Halmashauri hiyo imefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kati ya wilaya tisa za Mkoa wa Mara.

Pongezi hizo zimetolewa leo Septemba 25, 2026, na Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Bunda wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani, akisema matokeo hayo yanaonesha jitihada zinazofanywa na Halmashauri katika kuboresha sekta ya elimu

Katika mtihani huo, watahiniwa 2,845 walifanya mtihani, ambapo watahiniwa 2,399 sawa na asilimia 82 walifaulu kwa daraja la kwanza hadi la nne.

Sauti ya Daniel Yona diwani kata ya Kabasa
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bunda

Kwa upande wake, Afisa Elimu Sekondari wa Bunda amesema wameweka mikakati mbalimbali kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaendelea kuimarika katika mitihani ijayo.

Amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni kuweka utaratibu wa kufuatilia wanafunzi wanaokosa shule kwa kutumia barua zitakazosainiwa na wazazi, huku ufuatiliaji ukifanyika kuanzia ngazi ya kata hadi Halmashauri ya Mji wa Bunda.

Sauti ya Sauda Mwakyembe Afisa Elimu Sekondari Bunda TC