

20 June 2025, 9:35 am
Mambo ya kuzingatia nipamoja na AMCOS kutochezea mizani, wananchi kutobeba au kuhifadhi pamba kwenye sandarusi na makampuni kujitahidi kununua pamba kwa ushindani.
Na Adelinus Banenwa
Zikiwa zimetimia siku 20 tangu kufunguliwa kwa msimu wa ununuzi wa zao la pamba wilayani Bunda bei ya pamba yafikia 1200.
Akizungumza na Radio Mazingira Fm mkaguzi wa zao la pamba wilaya ya Bunda Ndugu Hemedi Kabea amesema bei ya ununuzi wa zao la pamba wilayani Bunda kwa sasa ni shilingi 1200 na hii inatokana na ushindani wa makampuni ya ununuzi wa zao hilo.
Katika hatua nyingine Kabea amesema kama serikali kupitia bodi ya Pamba wanafuatilia kwa karibu sana kuhakikisha kila mmoja anafuata miongozo iliyotolewa katika ununuzi wa zao la pamba msimu wa 2025 na 2026.
Akigusia baadhi ya mambo yaliyopo kwenye muongozo huo amesema kwa upande wa AMCOS kutokuchezea mizani, kuanza kununua pamba kwa bei mpya tu pale bei inapobadilika, na kwa upande wa wakulima Kabea amewasihi kuhakikisha wanazingatia usafi wa pamba ikiwemo kutoweka pamba kwenye sandarusi