Mazingira FM

Akutwa amepoteza maisha kwenye pagale ”wananchi wafunguka”

23 August 2023, 3:44 pm

Wakazi wa mitaa ya Nyasura C na Manyamanyama Mbugani wakiwa eneo la tukio , Picha na Adelinus Banenwa

Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 10 hadi 12 amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa katika jengo Moja la shule ya Elly’s iliyopo mtaa wa mbugani kata ya manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara

Na Adelinus Banenwa

Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 10 hadi 12 amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa katika jengo Moja la shule ya Elly’s iliyopo mtaa wa mbugani kata ya manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara

Mtoto huyo jinsia ya kike amekutwa jioni ya tarehe 22 Augost 2023 na wasamalia wema waliokuwa wakipita karibu na jengo la shule hiyo ambalo kwa Sasa halitumiki Kisha kuujulisha uongozi wa shule ambao pia ulitoa taarifa kwa viongozi wa serikali.

Akizungumza na redio Mazingira fm Mariam Chamba mkuu wa shule ya sekondari ya Elly’s amesema amepokea taarifa za kuwepo kwa mwili wa mtoto ndani ya Moja ya majengo ya shule ambayo hayatumiki majira ya saa kumi na moja na nusu jioniĀ  na alipofika na kuona uwepo wa mwili huo aliwasiliana na mmiliki wa shule pamoja na viongozi kwa hatua zaidi.

Mariam Chamba mkuu wa shule ya sekondari ya Elly’s

Naye diwani wa kata ya manyamanyama Mhe Mathayo Machilu ameiambia Mazingira fm kuwa tukio Hilo nilakusikitisha na eneo Hilo la Elly’s limeonekana kuwa hatari kutokana na kuwepo kwa majengo mengi ambayo hayatumiki hivyo yapo kama magofu jambo linaloweza kupelekea uharifu kutendeka.

Diwani wa kata ya Manyamanyama Mhe Mathayo Machilu

Kupitia mkuu wa kituo cha polisi Bunda OCS Magoti amewataka wananchi wawe makini na eneo hilo kutokana na muonekano wake pia amewaasa wazazi kuzingatia malezi kwa watoto wao na kufuatilia Kila wanapokwenda ili kuongeza usalama.

Mkuu wa kituo cha polisi Bunda OCS Magoti

Wakazi wa mitaa ya nyasura C na Manyamanyama Mbugani wameelezea kusikitishwa na tukio hilo na hasa maeneo tukio hilo lilipotokea wakidai usalama wake ni mdogo.

Wakazi wa mitaa ya Nyasura C na Manyamanyama Mbugani