BUNDA – mwingine apoteza maisha kwa kuliwa na mamba
12 December 2021, 1:51 pm
Bahati Galaya 32 mkazi wa Myatwali kijana aliyeshikwa MAMBA eneo la Nyatwali mtaa wa Kariakoo Halmashauri ya Mji wa Bunda usiku wa kuamkia ijumaa ya tarehe 10 dec 2021 amepatikana akiwa amepoteza maisha
Akizungumza na Redio mazingira fm mwenyekiti wa mtaa wa Kariakoo kata ya Nyatwali ndugu Jumanne Abdallah maarufu mzeea Makamaba amesema sasa umefika muda wa serikali kuwavuna mamba hao maana saizi wanawavizia wavuvi hadi kuwarukia kwenye mitumbwi yao.
Madata Mabula ambaye alikuwa na marehemu Bahati siku ya tukio ameieleza Mazingira fm juu ya tukio hilo namna lilivyotokea na kwamba kwa vyovyote vile ni ngumu sana kwa wavuvi wanaotumia mitumbwi midogo kujilinda na mamba hao kwa kuwa ni wakubwa.
Naye katibu tawala wilaya ya Bunda Salum Mtelela amesema baada ya tukio hili serikali haitakaa kimya badala yake amewaagiza TAWA na KDU kuhakikisha wanafanya doria kwenye mwambao wote wa ziwa Victoria katika eneo la wilaya ya Bunda ili kuwadhibiti mamba pia kuendelea kutoa elimu kwa wananchi
Ikumbukwe kwamba Bahati Galaya alishikwa mamba usiku wa kuamkia tarehe 10 dec 2021 akiwa katika harakati za kuvua samaki hadi leo asubuhi ambapo amepatikana akiwa amepoteza maisha huku ikitajwa ameacha mjane na watoto wanne bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe ameni
By Adelinus Banenwa