Mazingira FM

TAWA wafanikiwa kumuua mamba anayedaiwa kumuua mwananchi Nyatwali

20 February 2023, 2:59 pm

ASKARI wa wanyamapori TAWA wamefanikiwa kumuua mamba anayedaiwa kumuua mwananchi aliyekuwa akifanya shughuli za uvuvi mtaa wa Tamau kata ya nyatwali Halmashauri ya mji wa Bunda

Kutokana na maelekezo ya Ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda kwa askari ya TAWA aliyoyatoa mnamo tarehe 19 feb 2023 baada ya tukio la mkazi mmoja kushikwa na mamba aliwataka TAWA kutamtafuta mamba huyo ili asiweze kuleta madhara kwa watu wengine

Hata hivyo kupitia kwa Katibu Tawala wilaya ya Bunda Salum Mtelela amewataka wakazi wanaoishi kandokando ya ziwa Victoria ndani ya wilaya ya Bunda kuchukua tahadhari pindi wanapofanya shughuli zao kama vile kuchota maji, uvuvi n.k huku akiwataadharisha wavuvi kuacha kutumia mitumbwi midogo maarufu kama ”denge”