Mazingira FM

Mwanafunzi afariki kwa kugongwa na gari akielekea shule Bunda

22 November 2023, 9:00 am

Dinnah Matwiga (15) mwanafunzi wa kidato Cha kwanza shule ya Sekondari Pauljohn amefariki dunia kwa kugongwa na gari akielekea shuleni.

Na Adelinus Banenwa

Dinnah Matwiga (15) mwanafunzi wa kidato Cha kwanza shule ya Sekondari Pauljohn na mkazi wa mtaa wa Mashujaa kata ya Mcharo halmashauri ya mji w Bunda mkoani Mara amefariki Kwa kugongwa na gari wakati akielekea shuleni

Mwenyekiti wa mtaa wa Mashujaa Joseph Mifuko ameiambia Mazingira Fm kuwa tukio hilo limetokea saa Moja Asubuhi siku ya jumanne ya 21 November 2023 katika barabara ya balili mugeta ambapo mwanafunzi huyo akiwa na wenzake wakielekea shule alingongwa na gari hilo

Wazaza Elias baba mdogo wa Dinnah Matwiga amesema alipata taarifa ya tukio la ajari majira ya saa moja na nusu asubuhi na alipofika eneo hilo alikuta tayari binti yao amebebwa kupelekwa hospitali ya Bunda DDH na wakati akiwa njiani kuelekea hospitali alipewa taarifa kwamba Dinnah amefariki.

Wazaza ameiomba serikali kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani hasa Kwa maeneo yaliyoko nje ya mji ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

Juhudi zinaendelea za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Mara kutoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo.

Endelea kufuatilia vipindi vyetu na mitandao yetu ya kijamii.