Mazingira FM

Aliyejeruhiwa na mamba Chrismas afariki: Bunda

27 December 2023, 1:03 pm

Mmoja wa majeruhi wa tukio la kushambuliwa na mamba eneo la Mayoro kata ya Nyamihoro amefariki wakati akikibizwa hispitali ya mkoa

Na Adelinus Banenwa

Mmoja wa majeruhi wa tukio la kushambuliwa na mamba eneo la Mayoro kata ya Nyamihoro amefariki wakati akikibizwa hispitali ya mkoa.

Mfungo Magoma (48) mkazi wa Mayoro kata ya Nyamihoro wilayani Bunda aliyeshambuliwa na mamba siku ya tarehe 25 wakati akiendelea na shughuli ya uvuvi ziwa Victoria amefariki dunia wakati akipelekwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mara.

Afisa tarafa ya Kenkobyo Ndugu Boniphas Maiga amesema Mamba huyo alimjeruhi Mfungo maeneo mabaya ya mwili wake na alimvunja mfupa wa Nyonga hali iliyopelekea kuvuja damu nyingi.

Sauti ya Afisa tarafa ya Kenkobyo Ndugu Boniphas Maiga

Ikumbukwe kwamba Mfungo alikuwa amelazwa kituo cha Afya Cha Kasahunga Halmashauri ya wilaya ya Bunda kabla ya uamuzi wa kumuamishia hospitali ya mkoa ambapo alifariki wakati akiwa njiani kupelekwa hospitali.