Mazingira FM

DAS Bunda asisitiza usimamizi wa miradi na ukusanyaji mapato

16 May 2026, 5:13 am

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salum Mtelela

Mtelela ametoa rai hiyo wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2026/2027.

Na Mariam Mramba

Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salum Mtelela, amewakumbusha madiwani pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kuongeza kasi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha miradi iliyopo inakamilika kwa wakati na kuleta tija kwa wananchi.

Baadhi ya madiwani halmashauri ya wilaya ya Bunda

Mtelela ametoa rai hiyo wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2026/2027, kilichofanyika May 15/2026katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Baadhi ya watumishi halmashauri ya wilaya ya Bunda

Amesema Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda ipo tayari kushirikiana kwa karibu na madiwani pamoja na watendaji wa halmashauri katika kusimamia na kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hiyo.

Sauti ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, Salum Mtelela

Katika hatua nyingine, Katibu Tawala huyo amekemea tabia ya baadhi ya wanafunzi kutoka madarasani wakati wa vipindi kwenda kutafuta maji, akieleza kuwa hali hiyo inaathiri mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Kutokana na changamoto hiyo, amemuagiza Meneja wa RUWASA kuhakikisha anachukua hatua za haraka kutatua tatizo la upatikanaji wa maji katika shule mbalimbali, ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao bila usumbufu.