Mazingira FM

Aliyebaka ahukumiwa kupigwa viboko 6 na kuachiwa

13 April 2024, 6:34 pm

Mahakama ya wilaya ya Bunda

Mahakama ya willaya ya bunda imemuhukumu Mshtakiwa Frank Majani (18) kuchapwa viboko sita (6) baada ya kupatika na hatia kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa darasa la tano ambaye pia ni binamu yake.

Na Adelinus Banenwa

Jeshi la Magereza Bunda limetekeleza adhabu ya kuchapwa viboko sita iliyotolewa tarehe 08/ April /2024 na mahakama wilayani Bunda kwa Mshtakiwa Frank Majani (18) mkulima Mkazi wa Manyamanyama wilaya ya Bunda baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kubaka kinyume na Kifungu cha 130(1),(2),(e) na Kifungu cha 131(2),(a) cha KANUNI YA ADHABU SURA YA 16 MAREJEO YA MWAKA 2022, na kuamuru mshtakiwa huyo achapwe viboko sita (6) Kama sheria hiyo inavyooelekeza.

Awali ilielezwa mahakamani hapo na Mwendesha mashtaka upande wa Jamuhuri Athuma Salumu kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe 28/01/2023 majira ya mchana nyumbani Kwao na mshtakiwa ambapo alimbaka binti mwenye Umri wa miaka tisa (9) jina limehifadhiwa Mwanafunzi wa darasa la tano ambaye pia ni binamu yake.

Athumani Salumu alisema mshitakiwa na muhanga walikuwa wakiishi nymba moja hapo Manyamanyama ambapo muhanga alikuwa anaishi Kwa shangazi yake ambaye ni mama wa Mshtakiwa.

Hakimu Mkazi mwandamizi Betron Sokanya alisema upande wa mashtaka umethibitisha kosa hilo bila kuacha shaka yeyote hivyo kumtia mshtakiwa huyo hatiani na kumpa adhabu ya kuchapwa viboko sita, adhabu ambayo imetekelezwa leo mahakamani hapo na jeshi la Magereza mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi Betron Sokanya