Mazingira FM

PM Majaliwa aanza ziara mkoani Mara

2 March 2024, 5:31 pm

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasimu Majaliwa Majaliwa ziara yake mkoani Mara akianza na wilaya ya Bunda kwa kutembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasimu Majaliwa Majaliwa ziara yake mkoani Mara akianza na wilaya ya Bunda kwa kutembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Bunda.

Katika ziara yake hiyo kwa wilaya ya Bunda ametembelea na kukagua mradi wa shule mpya ya msingi Sabasita iliyojengwa katika kijiji cha Kihumbu kata ya Hunyari halmashauri ya wilaya ya Bunda iliyojengwa kwa thamani ya shillingi 348 milioni.

Katika halmashauri ya wilaya ya Bunda pia Mhe waziri mkuu amekagua na kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari ya wasichana ya mkoa wa Mara ( Mara girls secondary) inayojengwa kata ya Butimba Kijiji cha Bulamba halmashauri ya wilaya ya Bunda kwenye Jimbo la Mwibara inayojengwa kwa thamani ya shilingi bilioni 4 ambapo hadi sasa fedha iliyoidhinishwa ni shilingi bilioni 3 na majengo 23 yamejengwa kati ya majengo 27 yanatarajiwa kujengwa katika mradi huo huku shule hiyo ikitarajiwa kupokea wanafunzi kidato cha kwanza hadi cha sita.

Maelekezo ya Mhe waziri mkuu kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda ni kusimamia utekelezaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo inayopelekwa katika halmashauri hiyo huku akionesha kukerwa na tabia za udokozi na wizi katika miradi ndani ya halmashauri hiyo akitolea mfano mradi wa ujenzi wa hospitali ya halmashauri na wizi wa saruji zaidi ya mifuko 600 katika shule ya sekondari Mara girls.