Mazingira FM

UWT Bunda: Wanawake tumejipa kazi nyingi, tumesahau malezi kwa watoto

22 October 2023, 11:01 pm

Latifa Hamis, Mjumbe Kamati ya Utekelezaji CCM mkoa wa Mara. Picha na Edward Lucas

“Akina mama tumejipa shughuli nyingi tumesahau wajibu wetu wa malezi, twende tuwalinde watoto”

Na Edward Lucas

Wanawake wameaswa kuzingatia malezi ya watoto ili kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili ndani ya jamii

Wito huo umetolewa leo na Mjumbe Kamati ya Utekelezaji na Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara, Bi Latifa Hamisi wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Wanawake UWT Wilaya ya Bunda akiwa mgeni rasmi.

Latifa amesema licha ya majukumu mbalimbali wanayokabiliana nayo wanawake ndani ya jamii hawapaswi kusahau wajibu wao katika malenzi ya watoto huku akiwaasa pia kujitokeza katika kuwania nafasi za uongozi ngazi mbalimbali.

Wajumbe wa UWT Wilaya ya Bunda wakiwa katika kilele Cha Maadhimisho ya UWT. Picha Edward Lucas
Sauti ya Latifa Hamis
Evodia Zumba, Katibu UWT Bunda. Picha na Edward Lucas

Awali akizungumzia maadhimisho hayo Katibu wa UWT Wilaya ya Bunda, Evodia Zumba amebainisha shughuli mbalimbali zilizofanywa wiki hii ikiwa ni pamoja na shughuli iliyofanyika leo kwa kutembelea hospitali ya Manyamanyama kuonesha matendo mema kwa wagonjwa

Sauti ya Evodia Zumba