Mazingira FM
Mazingira FM
28 May 2026, 2:17 pm

Wakati mwingine magari hayo hutumika kubeba wanafunzi kwenda kwenye michezo na matamasha mbalimbali jambo ambalo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani.
Na Adelinus Banenwa
Imeelezwa kuwa ni marufuku magari ya mizigo ikiwemo malori kutumika kubeba abiria kutokana na hatari ya kiusalama
Akizungumza kupitia kipindi cha Asubuhi leo kinachorushwa na radio Mazingira FM katika mwendelezo wa utoaji elimu ya usalama barabarani SGT Amosi Masabo afisa wa usalama barabarani wilaya ya Bunda amesema kumekuwepo na tabia za baadhi ya watu kubebwa kwenye malori wekienda misibani wengine minadani.

SGT Amosi amesema wakati mwingine magari hayo hutumika kubeba wanafunzi kwenda kwenye michezo na matamasha mbalimbali jambo ambalo ni kinyume cha sheria za usalama barabarani.
Amesema jeshi la polisi wataendelea kuwachukulia hatua za kisheria ikiwemo kuwafikisha mahakamani madereva wa maroli watakaobainika wanabeba abiria kama kwenda misibani au wanafunzi au kwenye mikutano