Mazingira FM

DC Bunda atoa kongole kwa mbunge Maboto kusaidia madawati

4 October 2023, 3:58 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mh. Dkt. Vicent Naano. Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya Bunda Mh. Dkt. Vicent Naano amemshukuru mbunge wa jimbo la Bunda Mjini Robert Chacha Maboto kwa kusaidia shule za jimbo la Bunda Mjini kwa kutoa madawati 1049 zilizopatikana kutokana na fedha za mfuko wa jimbo.

Na Adelinus Banenwa

Mkuu wa wilaya ya bunda mhe Dkt. Vicent Naano amemshukuru mbunge jimbo la Bunda Mjini Robert Chacha Maboto kwa kusaidia shule za jimbo la Bunda Mjini kwa kutoa madawati 1049 yaliyopatikana kutokana na fedha za mfuko wa jimbo.

Dkt. Naano ameyasema hayo katika hafla ya kupokea madawati 100 kutoka bank ya NMB kwa ajili ya shule ya msingi Nyasura iliyopo kata ya Nyasura halmashauri ya mji wa Bunda.

Dkt. Naano amesema shule za Bunda mjini zina upungufu wa madawati elfu 6 huku wilaya nzima ya Bunda ina upungufu wa dawati elfu 16

sauti ya mkuu wa wilaya ya bunda mhe Dk vicent naano

Naye mkurugenzi wa mji wa Bunda Ndugu Emanueli Mkongo amesema shule zenye upungufu zaidi wa madawati ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda yakwanza ni Bigutu inayopatikana kata ya Bunda stoo na yapili ni shule ya msingi Nyasura.

Mkongo amesema katika vipaumbele watakuwa wanagawa dawati kadri ya uhitaji wa shule kulingana na namna zitakavyokuwa zinapatikana dawati hizo.

Sauti ya mkurugenzi wa mji wa Bunda Ndugu Emanueli Mkongo

Kwa upande wake katibu wa mbunge jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija amesema Mhe Mbunge wa jimbo la Bunda mjini kwa kushirikiana na mkurugenzi wa halamashauri ya mji wa bunda na ofisi ya mkuu wa wilaya wameadhimia kushirikiana na wadau wengine kupunguza adha ya madawati katika shule za msingi na sekondari katika jimbo la Bunda mjini.

Katibu wa mbunge jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija, Picha na Adelinus Banenwa
Sauti ya katibu wa mbunge jimbo la Bunda mjini Emmanuel Kija