Mazingira FM

Mbunge Maboto, akabidhi gari la wagonjwa kituo cha afya Wariku

22 February 2024, 12:50 pm

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Robert Chacha Maboto siku ya leo amemkabidhi Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Bunda, Emmanuel Mkongo gari mpya ya kubebea Wagonjwa itakayo toa huduma katika kituo cha afya Wariku.

Na Thomas Masalu

Akikabidhi gari hilo katika hafla iliyofanyika kituo cha afya ya Wariku kata ya Wariku, Mbunge Maboto ameitaka Halmashauri kutunza gari hilo ili kuhakikisha linadumu  kwa muda mrefu zaidi.

Aidha Maboto amewaomba viongozi wa chama na serikali kusimamia gari hilo ili litoe huduma inayotarajiwa kwa wananchi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkongo amesema kuwa wapo katika mchakato wa kukamilisha jengo la upasuaji ili kituo cha afya cha Wariku kianze kutoa huduma.

Hata hivyo katibu wa siasa na uenezi ccm wilaya ya Bunda, Gaspar Charles ameomba mkurugenzi kuendelea kusimamia ipasavyo miongozo ya serikali kuhusu utozaji wa fedha za mafuta katika gari la wagonjwa.