Mazingira FM

Vijana 72 kati ya 136 wameshindwa kuhitimu mafunzo ya jeshi la akiba ‘mgambo’ kata ya Nyamuswa wilayani bunda mkoani mara 2022.

14 October 2022, 5:01 pm

Vijana 72 kati ya 136 wameshindwa kuhitimu mafunzo ya jeshi la akiba ‘mgambo’ wilayani bunda mkoani mara 2022.

Utovu wa Nidhamu, Utoro, Uelewa na Kutomudu gharama za kulipia sare ni moja ya changamoto zilizopelekea baadhi ya wanafunzi kushindwa kuhitimu mafunzo ya jeshi la Akiba Wilaya ya Bunda yaliyofanyika kata ya Nyamuswa.

Hayo yamebainishwa kupitia Risala ya Wahitimu katika mahafari ya kufunga Mafunzo zilizofanyika jana tarehe 12 Oct 2022 katika viwanja vya shule ya Msingi Ikizu kata ya Nyamuswa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda Mkoani Mara.

Akisoma Risala hiyo mbele ya mgeni rasmi kwa niaba ya wengine, Peter Lugina Maunde amesema

Kwa upande wake mgeni Rasmi katika sherehe hizo ambaye ni Katibu Tawala Wilaya ya Bunda Kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya, Salumu Mtelela amewapongeza wahitimu na wakufunzi wa mafunzo hayo na kuahidi kushughulikia changamoto na maombi mbalimbali yaliyowasilishwa kupitia risala hiyo

Naye Mwakilishi wa Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Mara, Lieutenant Elias Laurent Orrota amewaasa wahitimu wa mafunzo hayo kuhakikisha wanatumia mafunzo waliopewa katika sehemu sahihi na kuondoa kasumba iliyojengeka kuwa mgambo ndio wamekuwa chanzo cha uhalifu mitaani.

Mafunzo hayo ya miezi minne na wiki mbili, wahitimu wamejifunza mambo mbalimbambali kama vile kwata za kijeshi, sheria, kanuni na matumizi ya silaha mbalimbali ili kuwasaidia kuishi kama askari pindi wawapo mtaani kwani uwepo wao utaisaidia serikali kutambua na kufichua magenge ya uhalifu na vitendo vingine viovu ndani ya jamii.