Mazingira FM

94 kati ya 154 wahitimu elimu ya msingi Tingirima

7 October 2023, 12:56 pm

Wahitimu wa darasa la saba shule ya msingi Tingirima. Picha na Taro M. Mujora

Na Taro M. Mujora

Shule ya msingi Tingirima iliyopo halmashauri ya wilaya ya Bunda mkoani Mara imefanya mahafali ya 42 ya kuwaaga wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi shuleni hapo.

Mahafali hayo yamefanyika jana Oktoba 6,2023 shuleni hapo huku mgeni rasmi akiwa ni diwani wa kata ya Ketare ambaye pia ni Mkurugenzi wa redio Mazingira Fm Mhe. Mramba Simba Nyamkinda.

Wahitimu katika risala yao iliyosomwa na Irene Emmanuel pamoja naye Hamisi Kitasho wamesema walianza elimu ya msingi mwaka 2017 wakiwa wanafunzi 154 na leo wanahitimu 94 sawa na asilimia 61, wavulana wakiwa ni 49 na wasichana wakiwa ni 45 na kubainisha changamoto mbalimbali zinazo ikabili shule hiyo ya msingi Tingirima.

Irene Emmanuel pamoja naye Hamisi Kitasho wakisoma risala.Picha na Taro M Mujora
Risala ya wahitimu shule ya msingi Tingirima

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Mwl. Nicholous Ayaga amesema shule inafanya vizuri kitaaluma na kupata mafanikio makubwa na kuifanya shule kung’ara mfurulizo kwa upande wa kitaaluma kwa mwaka 2017 hadi 2022 Isipokuwa mwaka 2018.

Mwl. Nicholous Ayaga, akisoma taarifa ya shule wakati wa mahafali kuwaaga darasa la saba. Picha na Taro M Mujora
Sauti ya Mwl. Nicholous Ayaga

Akitoa neno na kujibu risala ya wahitimu, mgeni rasmi Mhe. Mramba amesema wahitimu wanapaswa kujikita katika Elimu na Ujuzi huku akiahidi kutoa mifuko 10 ya saruji kwaajili ya kukamilisha chumba maalumu cha wasichana.

Mramba Simba Nyamkinda (wa kwanza kushoto) katika mahafali ya wahitimu darasa la saba shule ya msingi Tingirima.Picha na Taro Mujora
Sauti ya Mhe. Mramba Simba Nyamkinda