Mazingira FM

Bunda DC yamtunuku hati ya pongezi Meneja TARURA Bunda

12 December 2023, 5:06 pm

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Naano akikabidhi hati ya pongezi Kwa Meneja wa TARURA Bunda, na Adelinus Banenwa

Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Bunda limempatia hati ya pongezi Meneja TARURA wilaya ya Bunda Eng Baraka Mkuya.

Na Adelinus Banenwa

Baraza la Madiwani Halmashauri ya wilaya ya Bunda limempatia hati ya pongezi na fedha shilingi laki tano Meneja TARURA wilaya ya Bunda Eng Baraka Mkuya,

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Mhe Charles Manumbu amesema halmashauri hiyo imeamua kumtunuku hati hiyo ya pongezi kutokana na kazi nzuri anayoifanya hasa katika utengenezaji wa barabara na ufunguaji wa barabara mpya.

Mhandisi Barack Mkuya, Meneja TARURA Bunda akipokea mkono wa mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Naano

Akikabidhi hati hiyo ya pongezi Mhe mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Naano amesema ni jambo la kupongeza Kwa kazi kubwa anayoifanya Meneja TARURA

Aidha Dr Naano ametoa wito Kwa wakuu wa Taasisi za serikali na watumishi wengine kuiga anachokifanya meneja wa TARURA.

Kwa upande wake Meneja TARURA wilaya ya Bunda Eng Baraka Mkuya ameishukuru halmashauri ya wilaya ya Bunda Kwa kuona mchango unaotolewa na TARURA huku akibainisha kuwa hati hiyo ingawa imeandikwa jina lake lakini ni hati ya timu nzima ya TARURA.

sauti ya Mhandisi Barack Mkuya, Meneja TARURA Bunda