Mazingira FM

Mto wafurika, wanafunzi sekondari Sizaki wakwama kurejea nyumbani

24 April 2024, 9:52 am

Wanafunzi 26 wa sekondari ya Sizaki washindwa kurejea nyumbani baada ya kukuta mto umefurika maji.

Na Edward Lucas

Wanafunzi 26 shule ya sekondari Sizaki wameshindwa kurudi kwao Kisangwa April 23, 2024 na kulazimika kulala mtaa wa Mcharo baada ya kushindwa kuvuka mto Nyamawe uliofurika maji.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mtaa wa Sengerema, Gabriel Mwita Marwa amesema wanafunzi hao ambao wengi wanatokea maeneo ya Kisangwa wameshindwa kuvuka mto huo wakati wanatoka shule majira ya saa 12 kutokana na mto kufurika maji na hivyo kulazimika kulala kwa msamalia anayeishi ng’ambo ya pili ya mtoo mtaa wa Mcharo.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Sengerema, Gabriel Mwita Marwa

Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Mcharo Charles Maguta Bupumula ameiambia Mazingira Fm kuwa mto huo mara nyingi umekuwa ni tatizo kwa wanafunzi wanaotoka katika mitaa hiyo mitatu kwenda shule ambayo ni mtaa wa Mcharo, Sengerema na Kisangwa pindi mvua ikinyesha wakiwa nyumbani huwa hawaendi kabisa shuleni na ikinyesha wakiwa shuleni hulazimika kubaki wakisubili maji yapungue ili wavuke.

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Mcharo Charles Maguta Bupumula

Mazingira Fm imezungumza na msamalia huyo aliyetambulika kwa jina la Jumanne Mramba na kueleza kuwa alilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya kuona wanafunzi hao wamekosa namna ya kuvuka mto ambao unatishia usalama wa watoto hao hivyo kulazimika kuwapa hifadhi ya kulala.

Amesema wanafunzi hao 26, wasichana 23 na wavulana 3 amewapa nafasi za kulala katika nyumba zinazotumiwa na familia na kwasasa anaendelea na utaratibu wa kuwaandalia chakula.

Amesema wanafunzi hao 26, wasichana 23 na wavulana 3 amewapa nafasi za kulala katika nyumba zinazotumiwa na familia na kwasasa anaendelea na utaratibu wa kuwaandalia chakula

Baadhi ya wazazi wa watoto hao wamempigia simu na kumuomba awape hifadhi watoto hao hadi kesho yake hali itakapokuwa salama kwa wao kuvuka.

Sauti ya msamalia aliyewapatia hifadhi wanafunzi Jumanne Mramba