Mazingira FM

NMB yatoa msaada wa vifaa vyenye thamani ya shiling milioni 11 shule ya msingi Mihingo

16 December 2023, 1:58 pm

Bank ya NMB kama wadau wa maendeleo imetoa Mabati 182 shule ya Msingi mihingo na vifaa vingine vya kuezekea. Vyenye thanan ya shilingi 11 milioni.

Na Adelinus Banenwa

Bank ya NMB kama wadau wa maendeleo imetoa Mabati 182 shule ya Msingi mihingo na vifaa vingine vya kuezekea. Vyenye thanan ya shilingi 11 milioni

Msaada huo umetolewa Kwa lengo la kuonesha mshokamano na ushirikiano baina ya bank na jamii KUFUATIA madarasa matatu kati ya saba ya shule hiyo kuezuliwa na upepo.

Akizungumza kwakati wa kukabidhi msaada huo Meneja wa Bank ya NMB tawi la Bunda Ndugu Frances amesema Bank kama wadau wa Maendeleo wamechangia huduma mbalimbali katika sekta ya elimu na afya kama vile madawati na vifaa vya kuezekea Kwa upande wa elimu, na vitanda, magodoro na vifaa vingine vya kusaidia matibabu Kwa upande wa Afya.

Meneja huyo amesema bank hiyo pamoja na kupokea maombi mengi ya misaada lakini wao wamejikita katika sekta ya elimu, Afya na misaada katika wakati wa majanga Kwa kuwa wanaamini kupitia jamii ndipo wateja wao hutoka.

Meneja wa Bank ya NMB tawi la Bunda Ndugu Frances

Naye mbunge wa jimbo la Bunda Mhe Boniphas Mwita Getere amewashukuru benk ya NMB kama wadau wa karibu katika kutoa msaada pale wanapohitajika huku aiitajka ofisia ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya bunda kusaidia kukamilisha ujenzi wa madarasab .

Mbunge wa jimbo la Bunda Mhe, Boniphas Mwita Getere

Naye mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Bi Changwa Mkwazu ameishukuru Bank ya NMB kwa kuwa siyo mara yao ya kwanza katika kutoa misaada ambapo wamekuwa wakijitokeza kusaidia sit u kwa majanga bali hata kwenye mapungufu

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bunda Bi Changwa Mkwazu