Mazingira FM

Mbunge Maboto atoa vifaa vya milion 28 kwa wanafunzi Bunda mjini

8 January 2024, 8:51 am

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amekabidhi vifaa vya shule vyenye thamani ya shilingi mil 28 kwa wanafunzi wanaoishi kwenye mazingira magumu wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Na Adelinus Banenwa

Mhe Mbunge akisalimiana na baadhi ya watoto waliofika kupokea msaada wa vifaa vya shule

Mbunge wa jimbo la Bunda mjini Mhe Robert Chacha Maboto amekabidhi vifaa vya shule vyenye thamani ya shilingi mil 28 kwa wanafunzi wanaoishi kwenye mazingira magumu wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo mbele ya ofisi ya mbunge, Mhe Maboto amesema kama alivyoahidi kwenye kampendi za kugombea ubunge kwamba mshahara wake utarudi kwa wananchi ameendelea kufanya hivyo tangu alipochaguliwa kuwa mbunge wa ajimbo hili la Bunda mjini.

Moja ya watoto waliopata msaada wa vifaa vya shule kutoka Kwa Mbunge Maboto

Aidha amebainisha kuwa katika awamu hii ya kwanza ya ugawaji wa vifaa vya shule kwa mwaka 2024 wamenufaika watoto wapatao 240 ambao wamepatiwa vifaa vyote vya shule ambavyo ni madaftari, mabegi ya ashule, viatu, nguo za michezo, limu, miongoni mwa vifaa vingine.

SAUTI YA MBUNGE MABOTO
Mhe Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Naano

Kwa upande mwingine mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr Vicent Naano amesema ndani ya halmashauri ya mji wa Bunda ambayo ndilo jimbo la Bunda Mjini lenye kata kumi na nne, wanafunzi 4806 wanatarajiwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu hivyo amewataka wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanafika shuleni bila kikwazo hata kama hama sare za shule wala madaftari anatakiwa afike na kinyume na hapo wazazi au walezi watapelekwa mahakamani.

SAUTI YA DC NAANO