Mazingira FM

Serengeti Mara: Ajinyonga Baada ya kuthibitika kuwachinja watoto wake wanne

26 January 2022, 1:36 pm

Daud Samwel (30) mkazi wa Kitongoji cha Burunga Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara amejinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali yake baada ya kudhibitiwa kuwachinja watoto wake wanne kufuatia mke kumkimbia baada ya kuzidiwa na kipigo.

Tukio hilo limethitibitishwa na na jeshi la Polisi wilaya ya Serengeti.

Tukio hilo linadaiwa kutokea kati ya tarehe 24/01/2022 usiku mwili wake ulikutwa umening’inia kwenye mti jirani na kwake.

Mbabaji Aloyce ambaye ni jirani yake amesema,kabla ya uamzi huo alimpiga sana mke wake na kulazimika kukimbia,

”Tarehe 24/01/2022 saa 2 usiku alinigongea nikamfungulia akanambia kuwa mke wake amekimbia nimpe simu ampigie nikampa wakati huo sikujua kama ana panga mkononi,”

“Katika maongezi yake kwenye simu akasema,kwa kuwa umekimbia sasa naenda kuchinja mtoto mmoja mmoja tuone kama hutokuja kuwaona,kwa kuwa alikuwa amelewa gongo na inasadikika alikuwa anavuta bangi nikalazimika kumbana asiende kufanya unyama huo akawa mkali sana,” amesema jirani

Amesema,alilazimika kujitosa kumdhibiti wakavurugana na kuanguka chini akajaribu kuchomoa panga akambana ili asimkate na watu wakajitokeza wakafanikiwa kumpora panga,hata hivyo aliendelea kubainisha adhima yake lazima aue.

“Niliazimika kumpigia simu Ocd na balozi akataarifiwa,polisi hawakuchukua muda wakawa wamefika kwake hakuonekana ikawalazimu kuondoka na watoto na mama yao kwa ajili ya usalama wao,asubuhi nimeondoka bila kujua chochote baadae naambiwa kafa kwa kujinyonga,”amesema jirani.