Mazingira FM

Mapya yaibuka kifo cha mtoto aliyekutwa jengo la shule, wazazi wafunguka

24 August 2023, 1:32 pm

Wakazi wa maeneo ya Manyamanyama mtaa wa Mbugani wakiwa eneo ambalo mwili wa mtoto ulikutwa Picha na Adelinus Banenwa

Mwili wa mtoto aliyekutwa amefariki dunia maeneo ya shule ya sekondary ya Ellys iliyoko mtaa wa Mbugani kata ya Manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda umetambuliwa.

Na Adelinus Banenwa

Mussa Iramba mkazi wa Hunyari ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo ameiambia Mazingira fm kuwa ni kweli huyo ni mtoto wake anaitwa Suzana Iramba mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kabarimu na kwa kipindi kirefu alikuwa akiishi na shangazi yake maeneo ya majengo kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda,

Mussa amesema taarifa za kifo cha mtoto huyo amezijua kutoka kwa mama yake ambaye alimpigia simu majira ya saa saba za mchana kisha kwenda polisi kutoa maelezo ambapo aliambiwa kwenda chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.

“nimepigiwa simu na maama yake nikiwa hospitali ya DDH kwa kuwa nina mgonjwa anasubili kufanyiwa upasuaji mama yake na huyu mtoto akaniambia suzana amefariki amekutwa kwenye majengo ya shule ya Elly’s nimeshtuka ndipo nilichukua jukumu la kwenda polisi kutoa maeleza na polisi wakaniambia niende kituo cha afya bunda kuutambua mwiuli kama kweli niwamtoto wangu”

Mussa  ameendelea kuiambia mazingira fm akuwa ”ni kweli nimefika kituo cha afya chumba cha kuhifadhia maiti nikakuta kweli ni mwanangu roho inaniuma sana ukiangalia huku ninamgonjwa alafu napata habari kama hizi za msiba ”

Mussa Iramba baba mzazi wa mtoto

Kwa upande wake Estar Boniphas mama mzazi wa suzana amesema taarifa za mtoto huyo kufikwa na umauti alizipata kupitia kwa jeshi la polisi mapema leo asubuhi ambao walikuwa na taarifa za kupotea kwa mtoto huyo tangu tarehe 7 AUGOST ambapo walimwambia afike kituo cha afya bunda na alipofika alipelekwa mojakwa moja chumba cha kuhifadhia maiti ndipo alipogundua mtoto wake amefariki.

Estar Boniphas mama mzazi wa suzana

Radio Mazingira fm ilimtafuta shangazi wa Suzana ambaye ni Mankuru Mlasi mkazi wa mtaa Majengo kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda ambapo amesema taarifa za kifo cha Suzana alizipata tarehe 23 Aug 2023 majira ya saa saba mchana wakati akijiandaa kwenda kumuona mgonjwa wake hospitali.
Wankuru ameiambia mazingira fm kuwa ni kweli yeye amekaa na mtoto Suzana tangua akiwa anasoma darasa la pili hadi amefika darasa la sita na alimchukua kutoka kwa baba yake huko Hunyari na kuanza kuishi naye.
“Ni kweli mtoto huyu nilimchukua kwa baba yake akiwa darasa la pili na nimekaa naye katika kipindi chote hadi amefika darasa la sita lakini amekuwa na tabia ambazo siyo nzuri wakati akiwa kwangu amewahi kuletwa hapa kwangu mara tatu usiku akiwa ameokotwa mtaani siku nyingine aliletwa na mwenyekiti”
Wankuru ameendelea kuiambia mazingira fm kuwa baada ya kuona tabia ya mtoto imezidi hasa ya kushindwa kusoma kutaka kukaa mtaani na udokozi aliamua kumrudisha kwa baba yake huko hunyari na kusaini kwa mwenyekiti kwamba mtoto huyo hayuko tena mikononi mwake.

Wankuru Mlasi shangazi wa Suzana

Mawazo Mussa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo kata ya Kabarimu amesema ni kweli mtoto huyo anamfahamu na amewahi kuletwa kwake kama mara tatu akiwa ameokotwa mtaani usiku na alikuwa akimrudisha kwa shangazi yake ila kilichoonekana kwa mtoto huyo ni kukataliwa na kukosa malezi kutoka kwa wazazi na ndugu jambo lililopelekea mtoto huyo kuishia mtaani.

Mawazo Mussa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo

Ikumbukwe kwamba mwili wa suzana iramba ulipatikana tangu jana majira ya saa kumi na moja na nusu za jioni kwenye jengo moja la shule ya Ellys ambalo halitumiki ukiwa umetelekezwa.