Mazingira FM

Ofa ya zuku neema kwa wakazi wa Mara na mikoa jirani

25 April 2024, 1:11 pm

Wawakilishi kutoka zuku wakiwa studio za radio Mazingira Fm wakitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu huduma wanazotoa, Picha na Adelinus Banenwa

Zuku yaombwa kufikisha huduma vijijini kutatua changamoto ya vingamuzi kuganda kipindi cha masika.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa uongozi wa kampuni ya  zuku kufikisha huduma ya visimbuzi vyao  vijijini ili nao wanufaike na huduma zao.

Wito huo umetolewa na baadhi ya wasikilizaji wa radio Mazingira Fm kupitia kipindi cha Asubuhi leo ambapo viongozi wa zuku mkoa wa Mara na Mwanza walifika kufafanua masuala mbalimbali kuhusu utendaji wa visimbuzi hivyo.

Sauti ya maoni ya wananchi

Jawadi Karangi meneja wa zuku mkoa wa Mara amesema kwa sasa zuku inazo chanel nyingi, na hivyo kwa kutambua mchango na umuhimu wa wateja wao kwa sasa wanayo ofa ya gharama ya  kisimbuzi ni  shilingi elfu 48,000 kikiwa na kifurushi cha juu kabisa bure kwa mwezi mzima, ukilinganisha na shilingi lfu 58,000 gharama ya kawaida.

Wawakilishi kutoka zuku wakiwa studio za radio Mazingira Fm wakitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusu huduma wanazotoa, Picha na Adelinus Banenwa

Jawadu amesema kuwa mbali ofa hiyo pia kisimbuzi hicho kinaonekana kwa ubora katika mfumo wa HD hivyo hata walioko mabondeni watapata huduma bila usumbufu wa chanel kuganda au kukata.

Sauti ya Jawadi Karangi meneja wa zuku mkoa wa Mara

Aidha Jawadu amesema kupitia kisimbuzi (king’amuzi ) cha zuku unaweza kuzifuatilia redio mbalinbali ikiwemo radio Mazingira Fm.

Naye meneja wa zuku mkoani Mwanza Salum Amza amesema kisimbuzi chao kinaendelea kuwa bora kutokana na ofa mbalimbali walizonazo pia gharama nafuu za vifurushi ambapo kifurushi cha chini ni shilingi  9,999 tu huku kifurushi cha juu zaidi ni shilingi 27,500.