Mazingira FM

Mwanamke akutwa amejinyonga chumbani kwake Bunda

12 April 2024, 4:36 pm

Mwanamke mmoja liyetambulika kwa jina la Nyanjara Haruni Rubailo [48] amekutwa amefariki kwa kujinyonga nyumbani kwake Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Mwanamke mmoja liyetambulika kwa jina la Nyanjara Haruni Rubailo [48] amekutwa amefariki kwa kujinyonga nyumbani kwake Bunda.

Akizungumza na Mazingira Fm mwenyekiti wa mtaa wa Makumbusho kata ya Nyasura Ndugu Boniphas Musiba Mashenene amesema amepata taarifa za mtu kukutwa amejinyonga kutoka kwa ndugu wa mama huyo majira ya asubuhi ya saa moja.

Imedaiwa na mwenyekiti huyo kwamba mwanamke huyo alikuwa na watoto wake hadi usiku na ilipofika asubuhi saa kumi na mbili alitoka chumbani kwake na kwenda chumba cha watoto wa kike na baadae alirudi chumbani kwake hadi pale watoto walipogundua mama yao amekwisha jinyonga.

Mwenyekiti amesema Nyajara amekuwa akiishi na mume wake na watoto lakini kwa sasa mume wake anakaa Busekela kwa shughuli za utafutaji.

Boniphas amesema baada ya kupata taarifa alifika eneo la tukio kisha kuwajulisha jeshi la polisi ambao walifika mapema na baada ya taratibu zao wamekabidhi mwili kwa ndugu kuendelea na taratibu za mazishi.

Aidha mwenyekiti amesema katika uchunguzi marehemu Nyanjara hakuacha ujumbe wowote ambao unaonesha kwa nini ameamua kujinyonga lakini uwenda ni msongo wa mawazo.

sauti ya mwenyekiti Boniphas

Haruni Daudi Ibrahim ambaye ni mume wa Nyanjara [marehemu] amesema akiwa Busekera kwenye shughuli za utafutaji alipokea simu kutoka kwa kijana wake akisema mama yake amekutwa amejinyonga chumban kwake.

Haruni amesema amepokea taarifa hizo kwa masikitiko kwa kuwa mara ya mwisho alionana na mke wake wiki iliyopita wakati anaondoka kwenda Busekera na alimsindikiza akiwa anaonekana hana tatizo lolote Hadi alipopata taarifa za kifo chake.

sauti ya Haruni mume wa mama aliyekutwa amejinyonga