Mazingira FM

Watoa huduma wanaouza damu salama wapewa onyo

14 June 2025, 4:21 pm

Pakti za damu Picha kutokea mtandaoni

Damu inakaa salama ndani ya siku 35 tu na ikizidi hapo inakua si salama kwa matumizi.

Na Catherine Msafiri

Ikiwa Tanzania inaungana na mataifa mengine Duniani kuadhimbisha siku ya mchangia damu Mratibu wa Damu Salama wa Wilaya ya Bunda Bi. Betla Betramino,ameonya watoa huduma wenye tabia ya kuwauzia damu wananchi waache mara moja kwani damu salama haiuzwi bali inatolewa bure kwaajiri ya kusaidia wote wenye uhitaji

Ametoa onyo hilo leo 14 june ,2025 alipofanya mahojiano kwenye kipindi cha sema usikike kinacholuka kupitia radio mazingira fm ambapo amesisitiza kuwa wananchi wanatakiwa kutoa taarifa kwenye uongozi pindi wanapouziwa damu

Mratibu wa Damu Salama wa Wilaya ya Bunda Bi. Betla Betramino akimuhudumia mchangia damu,picha na Mgreth

Aidha Bi.Betla ameeleza kuwa mgonjwa anapokwenda hospital atakiwa apatiwe huduma kwanza ndipo atafutwe mtu wa kurudisha damu kwaajili ya kuja kusaida watu wengine

Pia ameongeza kuwa damu inakaa salama ndani ya siku 35 tu na ikizidi hapo inakua si salama kwa matumizi

Bi.Betla amesema kuwa damu inayotolewa haitumiwi wakati huo mpaka ifanyiwe vipimo ndipo inaweza kutumika

Mratibu wa Damu Salama wa Wilaya ya Bunda Bi. Betla Betramino

Hata hivyo Bi.Betla amebainisha kuwa kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda mpaka kufikia jana june 13 ,2025 wamekusanya chupa 102 za damu huku zoezi likiwa linaendea leo june 14,2025 mpaka saa 12 jioni

Mratibu wa Damu Salama wa Wilaya ya Bunda Bi. Betla Betramino