

28 May 2025, 6:38 pm
Amewataka wananchi na wanachama wa chama hicho kuwa makini na watu wanaotoka nje ya nchi na kutaka kuleta vurugu na chokochoko hapa nchini.
Na Adelinus Banenwa
Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Bunda ndugu Mohamed Juma Msafiri amewataka wananchi na wanachama wa chama hicho kuwa makini na watu wanaotoka nje ya nchi na kutaka kuleta vurugu na chokochoko hapa nchini.
Mohamed ameyasema hayo katika mtaa wa Mcharo kata ya Mcharo halmashauri ya mji wa Bunda kwenye hafla ya kumpokea mwanachama mpya kutoka chama cha wananchi CUF ndugu Dustan ambaye pia alikuwa mgombea wa kiti cha udiwani wa kata hiyo kwa mwaka 2015 na 2020.
Mohamed amewatahadharisha wanachama kuwa kumekuwepo na watu kutoka mataifa jirani wanaojiita wanaharakati lakini lengo lao likionekana ni kutaka kuvuruga amani ya nchi hivyo amewataka wananchi kutowaunga mkono.