Mazingira FM
Mazingira FM
3 November 2026, 12:44 pm

Kamishna Mkuu wa TRA atoa msamaha wa adhabu kuanzia mwezi October mpaka 31,December 2026 kwa wamiliki wa magari yaliyokiuka sheria na taratibu za forodha nchini
Na Catherine Msafiri
Wamiliki wa magari yaliyokiuka sheria na taratibu za forodha nchini wametakiwa kujitokeza kunufaika na msamaha wa adhabu uliotolewa na Kamishna Mkuu wa TRA kuanzia mwezi October mpaka 31,December 2026.
Maafisa wa Forodha mkoani Mara wameeleza muda ambao msamaha huo utaanza na kumalizika, huku wakitoa elimu kuhusu taratibu sahihi za kuingiza magari nchini ili kuepuka ukiukwaji wa sheria za forodha.
Akizungumza kwenye kipindi cha kapu letu radio mazingira fm Afisa forodha Mara Iddi Gubwe ametoa utaratibu unautumika wakati wa kuingiza magari nchi.
Aidha kwa upande wake Afisa Forodha Mara Pastory William amesema wamiliki wote waliokiuka taratibu za kisheria za forodha wanapaswa kufika ofis za TRA ili kupata msamaha huu ambao umetolewa.
Huku akiwakumbusha wamiliki wa magari binafsi na mashirika waliopewa vibari vya muda mfupi kuwa ni kosa kisheria kuuza au kubadili umiliki wa gari bila kukamilisha taratibu za kiforodha.