Mazingira FM

Bunda: Hofu ya kutekwa na ukatili kwa wanawake, msako waanza porini

28 August 2026, 9:45 pm

Wananchi wakiwa porini kumsaka mtu anayeshukiwa kufanya utekaji na ukatili kwa wanawake mkondo wa mto Rubana. Picha na Edward Lucas

Wananchi kwa kushirikiana na viongozi walazimika kuingia porini kumsaka mtu anayeshukiwa kuwateka wanawake, kuwatembeza uchi na kuwafanyia vitendo vya ukatili

Na. Edward Lucas

Wananchi wa Mtaa wa Mihale, Kata ya Mcharo na maeneo jirani wilayani Bunda, mkoani Mara, leo wamekusanyika na kuanza oparesheni ya kumsaka mtu anayeshukiwa kuhusika na matukio ya utekaji na unyanyasaji wa wanawake katika eneo hilo.

Hatua hiyo imekuja baada ya baadhi ya wanawake waliokuwa wamekwenda katika maeneo ya Mto Rubana kumkuta mwanaume wanayemshuku kuhusika na matukio hayo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Mihale, Manyama Magoiga, anaeleza hatua zilizochukuliwa na wananchi baada ya tukio hilo.

Sauti ya Mwenyekiti

Kwa mujibu wa mashuhuda, baada ya mwanaume huyo kubaini kuwa wananchi walikuwa wakijaribu kumkamata, alikimbia na kuvuka Mto Rubana na kuingia katika eneo la hifadhi upande wa pili wa mto huo.

Wananchi mtaa wa Mihale na maeneo jirani wakiendelea na msako wa wanaohusika na tukio la utekaji na ukatili kwa wanawake. Picha na Edward Lucas
Sauti za mashuhuda

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema matukio hayo yameendelea kuwapa hofu na wasiwasi, huku wakiziomba mamlaka kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha usalama wa wananchi unalindwa na kuwabaini wahusika wa matukio hayo.

Sauti za wananchi

Tukio hilo linafuuatia madai ya Agosti 22 mwaka huu, ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 18 alidaiwa kutekwa na kufanyiwa ukatili na mwanaume asiyefahamika katika eneo la Mto Rubana, baada ya kwenda kufua pamoja na wanawake wengine wawili, huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara likithibitisha kupokea taarifa na kuanza uchunguzi wa tukio hilo.