Mazingira FM
Mazingira FM
8 October 2026, 7:34 am

Jumla ya wanafunzi 105, wakiwemo wavulana 41 na wasichana 64, wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari katika shule hiyo
Na Taro Michael Mujora
Ukosefu wa bwalo la kulia chakula kwa wanafunzi na jiko la kisasa ni miongoni mwa mahitaji makubwa yanayoikabili Shule ya Sekondari Sizaki iliyopo kata ya Mcharo, Wilaya ya Bunda.
Mahitaji hayo yamebainishwa, Oktoba 7, 2026, katika taarifa ya shule iliyowasilishwa kwa mgeni rasmi wakati wa Mahafali ya 19 ya kidato cha Nne ya shule hiyo.
Akisoma taarifa ya shule mkuu huyo amesema jumla ya wanafunzi 105, wakiwemo wavulana 41 na wasichana 64, wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari katika shule hiyo kwa mwaka huu wa 2026.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Sizaki, Tarsila Masue, amesema pamoja na mafanikio mbalimbali, shule hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa jiko la kisasa, maabara za Biolojia na Kemia, pamoja na upungufu wa matundu ya vyoo.

Akijibu risala hiyo, mwakilishi wa Mbunge wa Bunda Mjini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Bunda, Marysiana Sabuni, amesema mbunge ameahidi ujenzi wa jiko la kisasa katika shule hiyo, lakini pia amewataka wazazi na walezi kuwahamasisha wanafunzi kufanya vizuri katika mitihani yao ya taifa inayotarajiwa kuanza Oktoba 19 hadi Novemba 6