Miundombinu ya usafiri Mkoani Geita yaboreshwa
29 March 2021, 5:14 pm
Watumiaji wa vyombo vya moto mkoa wa Geita wamesema hayati Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano watanzanaia Watamuuenzi kwa vitendo kwakuwa alisimamia na kuboresha Miundombinu ya usafiri.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa umoja wa magari madogo Tax Mkoa wa Geita Bw Charles Martin wakati akizungumza na Storm Fm katika kituo cha magari hayo ambapo amebainisha namna ambavyo jitihada kubwa zilizofanywa na hayati magufuli kwakusimamia vyema miundombinu ya usafiri.
Aidha watumiaji wa vyombo vya moto mjini Geita wamesema moja kati ya vitu ambavyo viliigusa nafsi zao ni pamoja na kudhibiti wizi kwenye vyombo vya usafiri hali ambayo imeleta amani kwa watanzania.
Hayati Dkt John Pombe Magufuli alihakikisha anasimamia miundombinu ya vyombo vya usafiri kwa kuweka miundo mbinu safi ya barabara sambamba na madaraja kama ambvyo alieleza wakati yupo Jijini Mwanza kwenye uzinduzi wa Daraja la Furahisha.