Storm FM
Storm FM
17 February 2026, 7:52 am

Mbunge jimbo la Geita mjini, mkoani Geita, Chacha Wambura amewapongeza wananchi kwa kujitoa kutengeneza miundombinu ya barabara huku akisema “katika kipindi cha uongozi wangu nitahakikisha barabara hii inatengenezwa kwa ubora zaidi ili kuondoa changamoto”
Na: Ester Mabula
Wananchi wa Kata ya Bung’wangoko wilayani Geita mkoani Geita wameungana na Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mhandisi Chacha Wambura kukarabati kwa kulima barabara ilioyopo katika kata hiyo.
Hatua hiyo imekuja kufuatia miundombinu kuwa mibovu hali inayopelekea ajali za mara kwa mara na kuathiri shughuli za kijamii na kiuchumi kama wanavyobainisha

Kufuatia jitihada hizo Mbunge Chacha ameahidi ndani ya kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake kuhakikisha anaboresha miundombinu ya barabara hiyo huku akiahidi tripu 50 za moramu pamoja na fedha taslimu kiasi cha shilingi laki 6 kwa ajili ya kuboresha zaidi eneo hilo.

Katika hatua nyingine ameeleza dhamira yake ya kuanzisha mradi wa kulima nyanya ambao utawanufaisha vijana akieleza kuwa lengo lake ni kuhakikisha vijana wanafanya kazi ili kujikwamua kimaisha
