Storm FM
Storm FM
13 February 2026, 12:28 pm

“Kwenye mkataba wetu hauoneshi kama sisi wapangaji tunatakiwa kuchanga pesa ili kuweza kuzibua choo, hili jambo linapelekea mkanganyiko” – mmoja wa mpangaji
Na: Kale Chongela
Choo kinachotumiwa na wapangaji 10 katika nyumba inayomilikiwa na Bi. Jedida Kassim iliyopo mtaa wa Ujamaa kata ya Kalangalala halamshauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita kimefungwa hali inayosabisha wapangaji hao kwenda kujisaidia kwa majirani.
Wapangaji hao wameiambia Storm FM kuwa choo hicho kimefungwa kwa muda wa zaidi ya siku 14 ambapo kwa mujibu wa maelezo yao wamesema mmiliki wa nyumba hiyo aliwataka wao kuchangia shilingi elfu 7 kila mmoja ili gari la takaa liweze kuvuta maji taka katika choo hicho.
Mmiliki wa nyumba hiyo amekiri choo hicho kufungwa na kufafanua kuwa changamoto ni baadhi ya wapangaji kutumia choo hicho vibaya ikiwemo kumwanga maji mara baada ya kufua nguo zao hali ambayo inachangia choo hicho kujaa mapema.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw. Musa Mbaruku amekiri suala hilo kutokea katika mtaa wake na kueleza kuwa baada ya kujiridhisha amemtaka mmiliki wa nyumba hiyo kufungua choo hicho ili wapangaji hao waweze kutumia.