Storm FM

Wafanyakazi wapongeza uwepo wa GGML Bonanza Day

9 February 2026, 10:55 am

Mgeni rasmi, Bw. Dominic Marandu akimkabidhi kombe Kapteni wa timu ya GGML baada ya kuibuka washindi. Picha na Ester Mabula

“Uwepo wa bonanza hili si tu kwaajili ya kucheza michezo mbalimbali bali ni kuimarisha afya za mwili pamoja na mahusiano miongoni mwa wafanyakazi” – Dominic Marandu, mgeni rasmi.

Na: Ester Mabula

Wafanyakazi wa GGML pamoja na kampuni zilizopo ndani ya mgodi huo wameshiriki katika bonanza la michezo lililofanyika Februari 07, 2026 katika uwanja wa Nyankumbu girls uliopo halmashauri ya manispaa ya Geita mkoani Geita.

Bonanza hilo limehusisha michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku, kukimbia kwenye magunia, kukimbia na yai kwenye kijiko, mchezo wa kukaa kwenye viti, basketball,netball, volleyball pamoja na mpira wa miguu kwa wanaume ambapo timu ya GGM iliibiuka mshindi katika mpira wa miguu kwa kuifunga timu ya Infinity bao 1 kwa 0.

Mchezo wa kutembea na yai kwenye kijiko ukiendelea kwa upande wa wanawake. Picha na Ester Mabula

Mgemi rasmi katika tamasha hilo Bw. Dominic Marandu ambaye ni Kaimu mkurugenzi wa Rasilimali watu kutoka GGM, amesema lengo la bonanza hilo ni kuimarisha afya pamoja na mahusiano miongoni mwa wafanyakazi.

Sauti ya Dominic Marandu, mgeni rasmi

Viongozi wa GGM Sports Club Gueen Irene Fele ambae ni katibu msaidizi na Mwenyekiti Valence Ibrahim wameushukuru uongozi wa Mgodi pamoja na uongozi wa shule ya Nyankumbu girls kwa kuweza kufanikisha uwepo wa bonanza hilo kwani limesaidia kuwakutanisha wafanyakazi pamoja  kwa lengo la kuimarisha mahusiano

Sauti ya Irene Fele, katibu msaidizi GGM Sports Club
Sauti ya Valence Ibrahimu, mwenyekiti wa GGM Sports Club
Mchezo wa kukimbia kwenye magunia kwa wanawake ukiendelea kwenye Bonanza la GGML. Picha na Ester Mabula
Baadhi ya wafanyakazi na wananchi waliojitokeza kwenye bonanza la michezo la GGML. Picha na Ester Mabula