Storm FM
Storm FM
5 January 2026, 12:58 pm

“Kunipigia kura na kunichagua ni kunikopesha maendeleo ndani ya miaka mitano na nitahakikisha changamoto zilizo ndani ya uwezo wangu zinakwisha” – Mbunge Lutandula
Na: Ester Mabula
Wananchi wa kijiji cha Nyantimba kata ya Nyarutembo halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita, wamemshukuru Mbunge wa Jimbo la Chato kusini Mhe. Paschal Lutandula kwa kuweza kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya sekondari iliyopo katika kijiji cha Nyantimba.
Wanafunzi katika kijiji hicho wamekuwa wakitembea umbali wa zaidi ya Kilometa 6 ili kupata elimu katika shule za maeneo jirani, ambapo wakizungumza kwa niaba ya wananchi wengineBi. Yuritha Panckras na Bw. Sylvanus Makeremo wametoa shukrani kwa mbunge huyo kwa kuweza kutatua changamoto hiyo.

Mkwasi Jonh ni Kaimu mkurugenzi halmashauri ya wilaya ya Chato amesema kuwa kwa muhula mpya wa masomo utakaoanza mwezi huu Januari jumla ya wanafunzi 75 wa kidato cha kwanza wataanza masomo katika shule hiyo.

Akizungumza baada ya kukabidhi mabati kwaajili ya ujenzi huo, ujenzi mbunge Lutandula amesema katika uongozi wake ataendelea kugusa wananchi wa jimbo hilo kwani wakati anaomba kura alikuatana na changamoto hiyo ya shule na kuahidi kuweza kuitatua ili kusaidia wanafunzi wa kijiji hicho kutotembea umbvali mrefu.
