Storm FM

Wakazi wa Nyakafuru wafurahia kituo cha afya

5 September 2025, 10:21 am

Jengo la kituo cha Afya Nyakafuru wilayani Mbogwe lililowekwa jiwe la msingi. Picha na Kale Chongela

Jumla ya miradi 9 ya maendeleo kwenye sekta ya afya, maji, elimu na miundombinu ya barabara wilayani Mbogwe mkoani Geita imepitiwa na Mwenge wa uhuru mwaka 2025.

Na: Kale Chongela

Wakazi wa kata ya Nyakafuru, halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mkoani Geita wamefurahia uwepo wa kituo cha afya katika eneo hilo kwani kitaondoa changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kiafya.

Hayo yamebainishwa na baadhi ya wananchi wa kata ya Nyakafuru baada ya kiongozi wa mbio za mwenge  wa uhuru kuweka jiwe la msingi katika kituo hicho cha afya.

Sauti ya wananchi wa Nyakafuru

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa  mradi wa kituo hicho cha Afya, Afisa mtendaji kata ya Nyakafuru amesema mradi huo unaenda kuwa mkombozi kwa wananchi wa eneo hilo na kwamba mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni mia moja katika utekelezaji wake.

Sauti ya mtendaji kata ya Nyakafuru

Kiongozi wa mbio  za Mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu Ismail Ally Ussi ameridhiwa na utekelezaji wa mradi wa kituo hicho cha afya na kwamba  lengo la serikali ya awamu sita ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya afya kwa ukaribu.

Sauti ya kiongozi wa mbio za Mwenge

Mwenge wa uhuru umezindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi 9 ikiwemo ya afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara wilayani Mbogwe mkoani Geita yenye thamani ya shilingi Bilioni 4.4.