Storm FM
Storm FM
1 September 2025, 5:53 pm

“Kwakweli tunaomba polisi wafuatilie tukio hili ili kukomesha watu wenye roho za kikatili na kinyama kiasi hiki, huyu mtoto huwezi jua angekuwa nani baadaye” – Mwananchi
Na: Edga Rwenduru:
Mtoto mchanga anayekadiriwa kuwa na siku moja amekutwa amechomwa moto na kutelekezwa kandokando ya barabara katika Mtaa wa Mwatulole Manispaa ya Geita mkoani Geita.
Tukio hilo limetokea leo Septemba mosi, 2025 ambapo wakizungumza kwa masikitiko makubwa baadhi ya wakazi wa mtaa huo wameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka ili kumpata mhusika aliyehusika na tukio hilo.
Jeshi la polisi lilifika eneo la tukio na kuchukua mwili wa kichanga hicho kwa ajili ya uchunguzi zaidi likifanya jitihada za kubaini aliyehusika na tukio hilo.
Taarifa ya mwandishi wetu inaeleza zaidi.