Storm FM
Storm FM
18 July 2025, 7:20 pm

Wanawake mkoani Geita wameendelea kuchangamkia fursa ya elimu ya ufundi katika vyuo mbalimbali vilivyopo mkoani humo ili kujikwamua kiuchumi.
Na Kale Chongela:
Zaidi ya wanawake 200 wakazi wa wilaya ya Chato mkoani Geita wanaonufaika na mafunzo ya ufundi stadi katika chuo cha VETA wilayani humo wameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya mafunzo hayo bila malipo.
Wanawake hao 240 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Chato wakizungumza na Storm FM chuoni hapo mbali nakuishukuru serikali kwa fursa hiyo wameahidi kutumia ujuzi huo kujikwamua kiuchumi nakusadia watu wengine.

Mkuu wa chuo cha VETA Chato Bi Liliani Mlimira amewapongeza wanawake hao kwa uthubutu huo huku akisema fani walizochangamkia ni pamoja na Uchakataji wa samaki,Upishi,Ufundi umeme na Ufundi bomba.
Mwenyekiti wa Wanawake na Samia Mkoa wa Geita ambae ni Makamu mwenyekiti wa Wanawake na Samia Tanzania Bi Adelina Kabakama amewasihi wananwake hao kutumia mafunzo hayo kujikwamua kiuchumi.
