Storm FM
Storm FM
31 May 2025, 2:49 pm

Serikali wilaya ya Geita imesema haitawafumbia macho wananchi watakaobainika kuwa chanzo cha uchafuzi wa mazingira.
Na: Kale Chongela:
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 31, 2025 na mkuu wa wilaya ya Geita Mhe. Hashim Komba akiwa katika mtaa wa Mwatulole uliopo kata ya Buhalahala katika halmashauri ya manispaa ya Geita mara baada ya zoezi la usafi uliokutanisha Jeshi la polisi mkoa wa Geita, Idara ya uhamiaji, magereza na wananchi wa eneo hilo.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya manispaa ya Geita Ndugu Yefred Myenzi ametumia fursa hiyo kuwasihi wananchi kujenga desturi ya kila mmoja kufanya usafi katika maeneo yao ili kuondokana na magonjwa yatokanayo na uchafu .

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mwatulole Bw. Edward Misalaba amesema katika kutekeleza suala la usafi katika eneo hilo ameunda kamati tendaji ya ufuatiliaji wa mwenendo wa usafi.
Ikumbukwe kuwa ni zoezi endelevu kupitia kampeni ya usafi wa mazingira ambayo imepewa jina la H’YAGULAGA GEITA ikimaanisha SAFISHA/FAGIA GEITA .
