Storm FM
Storm FM
6 May 2025, 5:12 pm

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani, wauguzi wilaya ya Bukombe waadhimisha siku hiyo Mei 03, 2025.
Na: Edga Rwenduru:
Chama cha wauguzi Tanzania (TANA) wilaya ya Bukombe mkoani Geita kimeiomba serikali kuwatatulia changamoto ya uhaba wa nyumba za watumishi katika zahanati nyingi zilizopo katika wilaya hiyo jambo ambalo linahatarisha usalama wao majira ya usiku pindi wanapoitajika kutoa huduma kutokana na kuisha mbali na vituo vya kazi.
Akisoma taarifa ya chama hicho mbele ya mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Shigela aliyekuwa mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani katika wilaya hiyo Leodgard Marco ambaye ni katibu wa TANA wilaya ya Bukombe amesema licha ya changamoto hiyo bado wanakumbana na changamoto ya upungufu wa wauguzi.
Aidha katika hatua nyingine mganga mkuu wa wilaya ya Bukombe Dkt. Deograsia Mkapa ameitaka jamii kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wauguzi

Mkuu wa mkoa wa Geita Martine Shigela amewahakikishia wauguzi na wafanyakazi wote wa sekta ya afya wilaya ya Bukombe kuwa serikali itafanyia kazi changamoto hizo
Maadhimisho ya siku ya wauguzi katika wilaya ya Bukombe yaliongozwa na Kaulimbiu isemayo WAUGUZI NI SAUTI INAYOONGOZA,WEKEZA KATI UUGUZI HESHIMU HAKI ,LINDA AFYA.
