Storm FM
Storm FM
18 April 2025, 4:43 pm

“Mama mzazi wa marehemu amepoteza maisha baada ya kupata mshtuko kutokana na taarifa ya kifo cha binti yake” – Mwenyekiti
Na: Edga Rwenduru:
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la Lesine Chongela, mkazi wa kijiji cha Bugogo kilichopo Kata ya Bukoli, wilaya ya Geita anadaiwa kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wake.
Tukio hilo lilitokea siku ya Jumapili tarehe 13 Aprili, majira ya saa saba mchana ambapo kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamebainisha kuwa walimkuta marehemu akiwa amelala ukutani huku mume wake akiwa amejichoma kisu tumboni.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bugogo B, George Elias Kubanda, ameeleza kuwa mama mzazi wa marehemu naye alipoteza maisha kutokana na mshtuko baada ya kupata taarifa za kifo cha mwanae.

Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Bukoli, Faraji Seif, amesema baada ya kufuatilia kwa kina sababu za tukio hilo, inasadikika kuwa chanzo ni wivu wa kimapenzi na mgogoro wa muda mrefu kati ya wanandoa hao.
Mwanaume aliyeusika na tukio hilo alikimbizwa kituo cha afya Nayarugusu kwa matibabu huku akiwa chini ya jeshi la polisi kwaajili ya uchunguzi.
Hivi karibuni Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Geita SACP Safia Jongo akiwa Mamlaka ya mji mdogo wa katoro alibainisha kuwa changamoto kubwa wanayopambana nayo kwa sasa ni mauaji yanayosababishwa na wivu wa kimapenzi